Makala
MBINU ZA KUOMBEA MAISHA YALIYOKWAMA
| Makala
MAOMBI YA KUONDOA ROHO INAYOKUKWAMISHA USIFANIKIWE MAISHANI:
Hii ni moja kati ya maombi muhimu unayopaswa kuyaomba kila wakati kwa kupata msaada wa kuvuka hapo ulipokaa na kudumu kwa muda mrefu.
Sio hard working ama kufanya kazi kwa bidii ndio kutakufanikisha, japo sio vibaya kufanya kazi kwa bidii - jitahidi kunielewa vyema.
Unaweza ukaweka bidii yako na juhudu yako mahali unapojisikia kuiweka ukitegemea utapata matokeo sawasawa na juhudi zako,lakini ukweli ni kwamba you will be dissapointed,matokeo yatakukatisha tamaa.
Ipo roho ambayo huachiliwa na adui kwenye maisha ya watu kwa lengo la kuwakwamisha kimaisha,na wajikute wapo palepale kwa kipindi kirefu pamoja na kwamba ndani yao wanasikia kabisa muda umefika wa wao kutoka kwenye hayo mazingira.
Wangapi wenu mnaona kabisa muda umefika wa kutoka!! Kuacha hayo mazingira na kuingia kwenye majira mapya!! Hali ya nje inaweza isikupe ushirikiano lakini ndani yako na moyo wako unakueleza kabisa kwamba enough is enough na kuba hatua yako inayohitajika ili hatimaye uvuke ulipo.
Roho ya kukwamisha maisha ya watu inaweza kukupata ukajikuta ndoa inagoma kabisa kufanikiwa kwako, mafanikio ya kiuchumi yanashikiliwa na adui pamoja na juhudi na bidii zako za mapambano kiasi cha kwamba ukiyaangalia maisha yako unaona kabisa kuwa hayo sio maisha yako.
Ok, maisha yako yamefichwa wapi? Nani anayo kwasasa? Utumie njia zipi kuyapata maisha yako na kuanza kuyaishi?
Umeshawahi kukutana na hii hali kwamba unajiona kabisa kuwa ulitakiwa kuwa hatua fulani kimaisha ila bado umekwama mahali? Unajiona kabisa ni kama umechelewa!! Kinachoongezeka kwako ni umri tu ila matokeo ya mafanikio uko palepale!!!
Tunatakiwa kuomba, tena sio kuomba kiukawaida, maana kama umeomba na bado umekwama, maana yake tuongeze nguvu na mbinu za kuomba kwetu ili tuone matokeo sahihi na majibu yapatikane…
Amka na mimi kila siku usiku saa SITA na tunakuwa Live kupitia channel yetu ya SIRI ZA BIBLIA.
Lolote kuhusu ushauri,maombi na maombezi ni sahihi kuwasiliana na madhabahu kwa namba +255 758 708804 popote ulipo duniani.
Pastor Innocent Mashauri
Maarifa ya Ki-Mungu
SADAKA